Uundaji Na Utekelezaji Wa Kazi-Mipango Ya Kukinga Na Kuzuia Itikadi Kali Za Ghasia Katika Afrika Ya Mashariki

Imechapishwa 10/08/2021
Waandishi: Patricia Crosby, Dominic Pkalya

Chombo hiki cha zana kimeundwa na Strong Cities Netwaork (SCN) kama rasilmali ya serikali (ikiwa pamoja na serikali za mitaa) na mashirika ya kijamii katika Afrika ya Mashariki yaliyo na hamu ya kuunda Mpango wa Mtaa wa Kuchukua Hatua (LAP). LAPs zinapania kujenga mitazamo ya sekta nyingi ya kuthibiti uwezo wa jamii wa kukabiliana na vianzo vya ghasia za kupindukia, uchochezi na chuki.

Chombo hiki cha zana kinajengwa kwa misingi ya tajiriba ya SCN katika kufanikisha mipango ya kinyumbani na kusaidia mipango ya hatua za maendeleo nchini Kenya, Jordan, Lebanon na Macedonia Kaskazini, pamoja na mazoea mema ya kimataifa kutoka kwa mitandao ya SCN katika zaidi ya miji 145. Mifano imetolewa kimsingi kutoka kwa miradi iliyofadhiliwa na SCN nchini Kenya na kusaidiwa na mifano mingine ya kimataifa ya SCN.

Msingi wa chombo hiki cha zana ni tajiriba ya Kenya ya kufanya Mkakati wa Kitaifa wa Kukabili Ghasia za Kupindukia uliozinduliwa 2016 uwe wa kinyumbani. Kielelezo hiki, ni mfano bora wa ushirikiano wa serikali kuu na serikali za mitaa katika P/CVE, maarufu kama Mpango wa Kaunti wa Kuchukua Hatua (CAP). Kielelezo cha CAP kinafanya kazi kama mazoea ibuka katika eneo la Afrika Mashariki na kuunganika na jitihada za kimataifa za LAPs.

Patricia Crosby ni Meneja wa Mipango katika ISD, akifanya kazi ya mipangilio yote ya SCN katika eneo la Afrika Mashariki. Alijiunga na ISD ili kuongoza upanuzi wa SCN katika Bara la Afrika na sasa anasaidia kaunti za Kenya ili kutekeleza CAPs zao kupitia kwa jitihada za kijamii za Multi-Year PROACT. Patricia anawajibikia uundaji wa ala za mafunzo, kusaidia katika kukuza ushirikiaano kati ya serikali kuu na mitaa na kutoa msaada wa moja kwa moja wa sera na mipangilio kwa mashirika ya kijamii na wadau wa serikali. Kabla ya hapa, Patricia alifanya kazi na Jumuiya ya Commonwealth katika kitengo cha Kukabili Itikadi Kali za Ghasia, kuunda na kutekeleza miradi ya serikali ya kujenga uwezo wa watu. Patricia pia amefanya kazi na serikali ya Canada, hasa kushughulikia migogoro, dharura za kibalozi na mipangilio ya maendeleo ya Mashariki ya Kati. Patricia alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa na Shahada ya Sayansi ya Kijamii katika Maendeleo ya Kimataifa na Utandawazi. Moja kati ya kazi zake za ISD/SCN ni hii ifuatayo:

https://strongcitiesnetwork.org/en/incorporating-new-approaches-our-approach-to-evaluating-p-cve-interventions/ 

Dominic Pkalya ni Meneja Mkuu wa Eneo katika ISD, akifanya kazi katika michakato yote ya ISD ya kukabili ugaidi nchini Kenya na eneo pana la Afrika Mashariki. Dominic pia anasaidia katika uundaji wa sera, utafiti, mafunzo na mbinu za ufuatiliaji na tathmini ili kupima athari za mipango ya kukabili ugaidi ndani na nje ya mitandao. Dominic anasimamia mipangilio ya kijamii ya PROACT ya kuingilia kati pamoja na kusaidia kazi za SCN na Young Cities nchini Kenya. Hapo mbeleni Dominic alikuwa msimamizi wa muradi unaodhaminiwa na USAID, unaoshughulikia uimarishaji wa nguvu za kijamii ili kukabili misimamo mikali katika eneo la pwani ya Kenya. Aliwahi kufanya kazi na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) Kenya, akiwa ametumwa kwa Mamlaka ya Kuzuia Ukame, akitoa msaada wa kiufundi wa kupunguza ghasia zinazotokana na silaha baina ya jamii za wafugaji nchini Kenya. Ana shahada ya uzamili katika Uanahabari, Mizozo na Masomo ya Amani kutoka katika Chuo Kikuu cha Umoja wa Kimataifa cha Amani na Shahada ya Sanaa katika masuala ya Serikali na Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Moi, Kenya. Baadhi ya kazi zake za ISC/SCN ni hizi zifuatazo:

https://strongcitiesnetwork.org/en/kenyan-stakeholders-call-for-implementation-of-local-action-plans-to-stem-youth-radicalisation-and-extremism/ 

https://strongcitiesnetwork.org/en/kenya-launches-new-community-based-interventions-programme/ 

https://strongcitiesnetwork.org/en/opinion-can-law-enforcement-be-a-positive-actor-for-change/

Dondosha ripoti