Uundaji Na Utekelezaji Wa Kazi-Mipango Ya Kukinga Na Kuzuia Itikadi Kali Za Ghasia Katika Afrika Ya Mashariki
Chombo hiki cha zana kimeundwa na Strong Cities Network (SCN), kwa misingi ya tajiriba ya Kenya katika uundaji wa Mipango ya Kaunti ya Kuchukua Hatua (CAPs) katika Kuzuia na Kukabiliana na Ghasia za Kupindukia, kama rasilmali kwa serikali na mashirika ya kijamii katika Afrika ya Mashariki yaliyo na hamu ya kuunda Mpango wa Mtaani wa Kuchukua Hatua (LAP).